
Bunge La Tanzania
The Parliament of the United Republic of Tanzania invites applications from qualified Tanzanians for the position of Secretary General of the Forum of Parliaments of Member States of the International Conference on the Great Lakes Region (FP-ICGLR). This position will be contested by candidates from three member countries: Tanzania, Kenya, and Burundi, as per the directives of the Troika meeting held on October 25, 2024.
NAFASI YA KAZI – KATIBU MKUU WA JUKWAA LA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KANDA YA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR)
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanda ya Maziwa Makuu (FP-ICGLR). Nafasi hii itagombewa na wananchi kutoka nchi tatu wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, na Burundi, kwa mujibu wa maelekezo ya kikao cha TROIKA kilichofanyika tarehe 25 Oktoba, 2024.
MAJUKUMU YA KATIBU MKUU
Katibu Mkuu ataongoza Sekretarieti Kuu ya FP-ICGLR, na atakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kusimamia masuala ya utawala, fedha, na usimamizi wa kiufundi wa shughuli za Jukwaa;
- Kuratibu shughuli zote za Jukwaa kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi mbalimbali ndani ya Jukwaa;
- Kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi ya Bunge la FP-ICGLR na mipango ya kimkakati ya Jukwaa.
SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu:
- Shahada ya kwanza (Bachelor’s Degree) kutoka chuo kikuu kinachotambulika.
Uzoefu:
- Uzoefu wa angalau miaka kumi (10) katika nafasi za uongozi wa juu katika taasisi za kitaifa, kikanda au kimataifa.
Uwezo wa Uongozi:
- Sifa za uongozi, uadilifu, na weledi wa hali ya juu.
Jinsia:
- Moja kati ya wagombea watatu wanaopendekezwa ni lazima awe mwanamke, kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wanapaswa kuwasilisha barua ya maombi, wasifu binafsi (CV), na nakala za vyeti vya elimu kwa njia ya barua pepe kupitia: cna@bunge.go.tz au
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro,
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli,
DODOMA.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni Ijumaa, Machi 14, 2025.
How to Apply
Applicants should submit a letter of application, a detailed resume (CV), and copies of educational certificates via email to:
- Email: cna@bunge.go.tz
- Parliament Office: 10 Morogoro Road, P.O. Box 941, 40490 Tambukareli, DODOMA.
- Application Deadline: Friday, March 14, 2025.