General Knowledge of WindSock: Uses and Importances

Windsock au Soksi za Upepo ni kifuata upepo au koni ya upepo.
Ni mfano wa mfuko wa duara uliotengenezwa kwa kitambaa maalum chenye umbile la mfano wa Soksi kubwa.

Windsock inaweza kutumika kama mwongozo wa msingi kuhusu uelekeo wa upepo na kasi sio kwenye viwanja vya ndege, bali hata kwenye viwanda hasa vya kemikali ambapo hutumika kutazama uelekeo hasa wakati wa hatari ya kuvuja kwa gesi.

Marubani na waongoza Ndege hutumia kifaa hiki na vingine kama #windvane kufahamu taarifa za uelekeo na kasi ya upepo katika viwanja vya ndege ili kushauri upande ambao ndege inatakiwa kuruka au rubani kuchagua mbinu ya kupaa ili kukinzana na msukumo.

Mara nyingi ndege hupaa au kutua kufuata upepo unapotokea (headwind) sio unapoelekea (Tailwind).

Katika viwanja vya ndege vingi windsock huwa ina angazwa na taa usiku iwe zilizoizunguka au iliyowekwa kwenye nguzo inayoangaza muonekano wake.

Mara zote upepo unapotokea ni kinyume cha windsock inapoelekea.
kwa hivyo upepo unapotokea kaskazini windsock itaonyesha kuelekea/kupepea kusini.

Windsock huwa inanyanyuka pale upepo unapovuma na kuinama pale upepo unapokuwa mdogo au hakuna mvumo.

Mistari inayoonekana kwa rangi ya machungwa na nyeupe hutumika kusaidia kukadiria kasi ya upepo.
Kila mstari unaashiria kasi ya mafundo 3 ya upepo (3 knots) au kilomita 5.5

Mfano:
Windsock ikinyanyuka mstari wa kwanza tu mwanzoni wenye rangi ya machungwa basi upepo una kasi ya fundo 3 au kilomita 5.5 kwa saa.

Ikinyanyuka mstari unaofuata wa pili mweupe tambua upepo una kasi ya fundo 6 au kilomita 11 kwa saa.

Inaendelea hivyo hadi mstari wa mwisho wa tano wenye rangi ya chungwa ambao kasi ya upepo ni fundo 15 sawa na kilomita 28 kwa saa.

Kumbuka Windsock haijawekwa tu kama bendera za mashabiki wa soka, bali imeainishwa katika kiambatisho cha 14 kwenye shirikisho la usafiri wa anga ulimwenguni #ICAO, pamoja na kanuni, miongozo au sheria za wadhibiti kutoka nchi tofauti ulimwenguni.

Soksi za Upepo huja kwa ukubwa tofauti wa urefu na kipenyo kulingana na matumizi yaliyokusudiwa.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) imeainisha ukubwa wa;
Urefu wa Mita 2.5 au futi 8 na kipenyo cha cha mita 0.45 mwanzo.

Ili kujulishwa ikitokea nafasi mpya unayoitafuta BOFYA HAPA